Jumanne, 17 Februari 2015

Girlfriend wa Ray J mikononi mwa polisi baada ya ugomvi wa kupigana…



Bifu la mwanamuziki Ray J na mpenzi wake Princess Love limeendelea kuchukua sura mpya na sasa limeibuka kwa mara nyingine miongoni mwa wawili hao.
Awali wawili hao waliachana huku mwanamke huyo akitamka kutaka kujiua baada ya kuachana kwao lakini baadaye walirudiana.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jumatano iliyopita kulizuka ugomvi kwa wawili hao walipokua hotelini na kupelekea Princess kumuumiza Ray J hadi kutokwa damu na kujikuta mikononi mwa polisi.
Tukio hilo lilitokea wakati Ray J alipokuwa akirudi hotelini akitokea katika club ya Strip joint ambapo walinzi wa hotel hiyo walisikia sauti ya msichana huyo ikidai “I’m gonna kill you”.
Lakini baada ya kushikiliwa na polisi kwa muda Ray J baadaye alimtoa kwa dhamana baada ya kumlipa mwanasheria wake dola 10K.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni